Majuto: Naumwa Tezi Dume.



King Majuto
Muigizaji wa wa Filamu na maigizo King Majuto amefunguka kuhusiana na ugonjwa unaomsumbua.
Akizungumza na MCL Digital ilizungumza naye jana jioni Jumanne na kukiri kwamba amegundulika ana tezi.
Msanii huyo anaendelea kupata matibabu Hospitali ya Tumaini iliyoko Upanga Jijini Dar es Salaam huku akisubiria hatua ya upasuaji.
Taarifa iliyotolewa  jana Jumanne na Chama cha Waigizaji  Mkoa wa Kinondoni ilieleza kuwa mwigizaji nguli,  Amri Athuman (King Majuto) amelazwa katika Hospitali ya Tumaini iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.
Mkongwe huyo anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa tezi dume wakati wowote kuanzia sasa baada ya kukamilisha vipimo vyote.
Ofisa Habari Uenezi Mahusiano na Umma, Masoud Kaftany aliwaomba wapenzi wa filamu na Watanzania wote kumuombea Mzee majuto ili hali yake iimarike.

Comments