
Katika majibishano hayo ya risasi yaliyodumu kwa zaidi ya saa mbili
watu watano wanaosadikiwa kuwa majangili sugu walizidiwa nguvu na
kujisalimisha mikononi mwa askari polisi na askari wa Hifadhi ya Taifa
ya Katavi.
Kamanda wa Polisi Katavi, Damas Nyanda alisema kuwa katika mapambano
hayo jeshi la polisi na askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi
walifanikiwa kukamata silaha nzito tatu aina ya SMG pamoja na magazine
tano na risasi 16.
Aliongeza kuwa pia walifanikiwa kukamata nyara za Serikali zenye
thamani ya Sh milioni 37.9. Kamanda Nyanda alisema nyara hizo ambazo ni
vipande vinne vya meno ya tembo kwa pamoja vikiwa na uzito wa kilo 6.6
vyenye thamani ya Sh milioni 35 na nyama ya pofu yenye uzito wa kilo 20
ikiwa na thamani ya Sh milioni 3.9 kwa pamoja viikuwa vimefichwa kwenye
mifuko ya sandarusi.
Kamanda Nyanda alisema kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa manane wa
kuamkia jana katika kijiji cha Kapalamsenga mwambao mwa Ziwa Tanganyika
wilayani Tanganyika. “Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na
askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi tulifanya msako kwa pamoja kwa wili
tatu tukiwasaka ‘majangiri’ hawa sugu usiku na mchana, ndipo
tulipobaini maficho yao nao wakajihami kwa kuanza kuturushia risasi na
ndipo mabishano makali ya risasi yalipotokea baina yao na sisi,” alieleza Kamanda Nyanda.
Alieleza kuwa watuhumiwa hao watano wanaendelea kuhojiwa ili kuweza
kubaini mtandao wao wa ujangiri ambapo watafikishwa mahakamani mara tu
baada ya uchunguzi wa awali wa kesi yao kukamilika. Kwa upande wake, Mku
wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi, Izumbe Msindai alisema ushirikiano wa
Jeshi la Polisi na askari wa Hifadhi hiyo umefanikisha kukamatwa kwa
watuhuimiwa hao.
Chanzo; HabariLeo
Comments