
Marehemu huyo, alionekana kichakani Ijumaa iliyopita saa 4:00 asubuhi
karibu na maeneo ya mashamba ya wanakijiji hicho baada ya ndugu
kutokumwona nyumbani kwao kwa muda wa siku saba na kutoa taarifa ofisi
za kijiiji.
Mwenyekiti wa kijiji hicho Josephat Mtayoba, alisema baada ya kupokea
taarifa za binti huyo na kuwasiliana na ndugu wa marehemu walisema
wakati akiondoka alikuwa anawasiliana na watu ambao ndugu zake
hawakuwafahamu.
“Kwa kijiji hiki ni tukio la kwanza kushuhudia mauaji ya
kushtua kama hatua zinazoendelea kuchukuliwa ni kuweka na kuimarisha
ulinzi shirikishi, “alisema Mtayoba.
Baba wa marehemu huyo Felix Gabriel , alisema binti yake, alitoka
shambani akiwa na jembe na kuliweka nyumbani kisha kuondoka akiwa
anaongea na simu, lakini hakufahamu alikuwa akiongea na nani.
Aidha alisema baada ya kukaa kwa muda mrefu akiwa haonekani nyumbani
alidhani kuwa mwanae atakuwa ameolewa hivyo anasubiri kupokea mahari
kutoka kwa wakwe.
“Aliondoka nyumbani tangu Januari 5, mwaka huu na mwili
wake kuokotwa na mdogo wake mchunguzi Felix Ijumaa iliyopita Januari 12
mwaka huu,”alisema Gabriel.
“Nilivyoona anaondoka sikushtuka kwani nilijua atarudi na
alivyokaa siku nyingi nilidhani atakuwa ameolewa nilijipanga kupokea
mahari ya binti yangu, “alisema Gabriel kwa uchungu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Agustine Ollomi, alithibitisha
tukio hilo na kusema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kuwatafuta
wahalifu hao na kwamba hakuna aliyenaswa.
chanzo:
Comments