Maadui wa Uislamu wapinga kutangazwa siku ya kupambana na chuki dhidi ya Waislamu nchini Canada.

Maadui wa Uislamu wapinga kutangazwa siku ya kupambana na chuki dhidi ya Waislamu nchini CanadaKundi la mrengo wa kulia la maadu wa Uislamu katika mji wa Quebec nchini Canada wamepinga ombi la Waislamu la kutangazwa rasmi siku ya kupambana na chuki dhidi ya Waislamu kama njia ya kukumbuka tukio la kushambuliwa kwa risasi msikiti wa Quebec.

Vyama vyenye chuki za kidini vya mrengo wa kulia nchini Canada vimetangaza kuwa, itabidi maneno "chuki dhidi ya Uislamu" yasitumike iwepo tukio hilo linataka kutambuliwa rasmi.
Baraza la Taifa la Waislamu nchini Canada limemuomba waziri mkuu wa nchi hiyo Justin Trudeau kuitangaza siku uliposhambuliwa kwa risasi msikiti huo kuwa siku ya kupambana na chuki dhidi ya Uislamu nchini humo kama njia ya kuwaenzi wahanga wa jinai hiyo.
Tarehe 31 Januari 2017, gaidi mmoja mwanachama wa makundi ya mrengo wa kulia yenye chuki za kidini aliwashambulia kwa risasi Waislamu waliokuwa wanasali katika kituo cha utamaduni cha Kiislamu mjini Quebec huko Canada na kuua Waislamu 6 na kuwajeruhi wengine kadhaa. 
Gaidi huyo aliingia msikitini humo wakati makumi ya Waislamu walipokuwa wanasali sala la Alasiri na kuanza kuwafanyatulia risasi ovyo.
chanzo:parstoday.

Comments