
Mchezaji
huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 24 baadaye alijiunga na
Manchester United kwa dau la pauni milioni 75 msimu wa uhamisho
uliopita.
Farhad Moshiri aliwaambia wenye hisa katika mkutano na
wachezaji kwamba mchezaji huyo alipokea ujumbe ''wa kwenda kuhiji
Afrika'' wakati ambapo alitarajiwa kutia saini mkataba mpya katika klabu
ya Everton.
''Alikuwa na uchawi na akapokea ujumbe aliotaka kwenda Chelsea'', alisema Moshiri.
Mabingwa
wa ligi ya Uingereza Chelsea walikuwa wamewasilisha ombi la kutaka
kumsajili Lukaku lakini badala yake akajiunga na Manchester United.
Mwezi Machi ajenti wa Lukaku Mino Raiola alikuwa amedai kwamba
mkataba mpya wa kusalia Everton ulikuwa umekamilika asilimia 99.9.
''Tulimpatia
kandarasi nzuri zaidi ya Chelsea na ajenti wake aliwasili kuja kutia
kandarasi'' , Moshiri aliambia mkutano wa kila mwaka wa Everton.
Bilionea
huyo wa Iran, Moshiri ambaye alikwa amewekeza dola milioni 150 katika
deni la klabu hiyo, alisema kuwa Everton ilimpatia mshambuliaji huyo
fedha nyingi ili kusalia.
''Swala la Lukaku halikuwa la kifedha.
Iwapo nitaendelea kuwa miliki mkuu wa klabu hiyo maswala ya kifedha
hayatakuwa tatizo''.Moshiri alisema kuwa Lukaku baadaye alimpigia simu
mamake kabla ya mchezaji huyo kufichua kwamba alipokea ujumbe
uliomwambia ajiunge na Chelsea.
chanzo:Bbc.
Comments