Yanga itaifuata Azam kwenye Uwanja wa Azam Complex katika pambano hilo la kumalizia duru la kwanza la Ligi Kuu Bara litakaloanza saa 10:00 jioni.
Katika mazoezi hayo ya jana, Kocha George Lwandamina aliyekuwa anasaidiwa na Noel Mwandila na Shardack Nsajigwa walisimamia mazoezi hayo kwa kutenga vikosi viwili huku, Buruan Yahya na Obrey Chirwa wakifunika kinoma.
Awali Kocha Mwandila alianza kumwaga ujuzi kwa vijana kabla ya Lwandamina naye kuongeza nguvu akisisitiza mambo ya msingi ya kumiliki mpira na kupiga mashuti ikiwa kama mbinu za kuelekea mchezo wao wa kesho.
Baada ya zoezi hilo Lwandamina alihama na kuwachukukua Mwinyi Haji, Papy Tshishimbi, Gadiel Michael, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Hassan Kessy, Said Makapu na Juma Abdul na kuwapa zoezi la kukaba na kushambuliana kwa pamoja.
Kabla ya timu hizo kugawanya pande mbili na kuangusha mbungi la dakika 30 ambapo matokeo yaliisha kwa mabao 2-1, kikosi cha Chirwa na Ajib kikiziwa ujanja na kile cha kiberenge Buruan Yahya aliyenoga kwa krosi zake zenye macho.
TAMBWE, MKOMOLA HATIHATI
Hata hivyo katika mazoezi ya jana straika Amissi Tambwe alishindwa kuungana na wenzake baada ya juzi kujitonesha goti lake na kuleta wasiwasi wa kulikosa pambano hilo la kesho.
Tambwe aliungana na Thabani Kamusoko kufanya mazoezi mepesi ya kukimbia uwanjani kwa kuzunguka kwa dakika 30.
Naye Straika Yohana Mkomola hakuweza kufanya mazoezi na wenzake,.aliumia katika pambano dhidi ya Ruvu Shooting.
CHIRWA AOKOA JAHAZI
Lakini sasa ni kwamba kurejea kwa Chirwa katika kikosi hicho kuitaifanya kutuliza presha ya mashabiki wa Yanga, baada ya kuonekana kuwa fiti.
Comments