Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo
imesema kuwa, kundi hilo la kigaidi linatekeleza mashambulizi yake kwa
kutumia jina la kundi la Daesh kwa lengo la kuzipotosha fikra za walio
wengi duniani.
Imeeleza kwamba, kundi la Haqqani linafanya harakati hizo
ili kuifanya serikali ya Pakistan iweze kusalimika na mashinikizo ya
fikra za walio wengi na pia mashinikizo ya nchi nyingine.
Hii ni katika hali ambayo mashambulizi
matatu ya umwagaji damu mkubwa hivi karibuni mjini Kabul na Jalalabad
yalipelekea karibu watu 100 kuuawa ambapo kundi la Daesh lilitangaza
kuhusika na hujuma hizo.
Kundi la Haqqani ni tawi la operesheni la kundi
la kigaidi la Taleban ambalo wanachama wake wamekuwa wakitekeleza
mashambulizi mengi katika maeneo tofauti ya Afghanistan dhidi ya
serikali na polisi ya nchi hiyo.
chanzo: parstoday.
Comments