
Lema ametoa kauli hiyo baada ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma kuwataka wanasiasa na viongozi wa serikali wenye mamlaka ya kikatiba na sheria kutoingia utendaji wa Mahakama na kuheshimu Muhimili huo.
“Mh. Jaji Mkuu kauli kuhusu wanasiasa na Watendaji wa Serikali kutokuingilia Mahakama ni kauli muhimu kwa wkt huu, lakini Mahakama ambayo ni imara katika haki inawezaje kukubali kuingiliwa ?Mahakama inapaswa kujitazama zaidi.Mahakama ikiyumba Taifa linayumba,”ameandika Lema kwenye mitandao yake ya kijamii.
Jaji Ibrahimu alisema hayo, January 23 mwaka huu jijini Dar es salaam, wakati akifafanua siku ya maadhimisho ya siku ya sheria nchini yatakayoadhimishwa Februali Mosi Mwaka huu.
chanzo:zanzibar24.
Comments