Suprise
ya nguvu imefanyika usiku wa kuamkia leo pale Hyatt Regency Hotel baada
ya Malkia wa Bongo Movies, Wema Seetu kumpandisha mkali wa Bongo Fleva,
Diamond Platinumz ukumbuni kwa ajili ya ufanya makamuzi.
Tukio
hilo limetokea wakati wa hafla ya kumtambulisha msanii mpya wa Lebo ya
WCB Wasafi, Mbosso ambaye amejiunga na lebo hiyo baada ya kundi lake la
awali la Yamoto band kuvunjika.
Wakati
sherehe ikiendelea, Rayvanny alikuwa akikamua, wakati akimalizia shoo
alimuita Wema Sepetu ambaye aliibuka jukwaani kisha zikaanza kusikika
kelele za mashabiki wakiimba …Wema…. Wema….Wema… ambaye baada tu ya
kupanda na kuwasabahi mashabiki alimuita mpenzi wake wa zamani, Diamond
Platinumz naye apande jukwaani.
Kelele
ziliongezeka …Diamond… Diamond… Diamond…., haikuchukua muda Diamond
akaibuka jukwaani na kukumbatiana na Wema kwa sekunde takribani 20 kabla
ya kuanza kukamua.
Wakati
Mond akikamua jukwaani na wasanii wengine wa WCB, Wema alikuwa akikata
mauno jukwaani hapo jambo ambalo liliamsha msisimuko na shangwe miongoni
mwa mwashabiki na kelele nyingi za kuwashangilia zikitawala.
Ikumbukwe
kuwa Wema na Diamond waliwahi kuwa wapenzi miaka kadhaa iliyoita kabla
ya kuachana na kila mtu kuingia kwenye mahusiano mengine.
Comments