
Dkt Tatu Kamau anasema sheria inayoharamisha ukeketaji wa wanawake na
wasichana inakiuka utamaduni katika jamii nyingi za Kiafrika.
kadhalika, amesema ni ubaguzi dhidi ya wanawake ikizingatiwa kwamba upashaji tohara wa wanaume unakubalika kisheria.
Daktari huyo anataka pia bodi ambayo iliundwa nchini humo kukabiliana na upashaji tohara wa wanawake ivunjiliwe mbali.
Aliwasilisha kesi hiyo katika Mahakama Kuu mjini Machakos, mbele ya
jaji David Kemei kwani kesi hiyo itaanza kusikilizwa mwezi ujao.
Dkt Kamau, akizungumza na wanahabari baada ya kuwasilisha kesi yake,
alisema wanawake wote, sawa na watu wazima popote pale, wanafaa
kuruhusiwa kufanya uamuzi kuhusu miili yao wenyewe bila kuwekewa vikwazo
na sheria.
Amesema raia wa nchi za Magharibi wanafanya jambo sawa na ukeketaji, kufanya upasuaji kwenye uke ni kurekebisha maumbile.
“Upashaji tohara ulikuwa sehemu ya utamaduni wa Waafrika kabla ya kufika kwa wakoloni na haifai kuharamishwa,” amesema.
“Punde tu itakapohalalishwa, tutaweza kufanya tohara kwa njia iliyo
bora Zaidi, mojawapo ikiwa njia ya hospitali. Tukifanya hivyo basi
itakuwa salama kabisa. Na njia hii ni mojawapo wa upasuaji wa kawaida
duniani kote.”
Anasema wanawake wengi wamekuwa wakisumbuliwa na maafisa wa dola au hata kufungwa jela kwa sababu ya ukeketaji.
“Ingawa tunataka sana kumlinda mtoto msichana, kuna wanawake wengi
sana ambao wamekamatwa na kufungwa katika kipindi cha miaka mitatu
iliyopita,” anasema.
“Unapokuwa mtu mzima, hakuna sababu yoyote ya kuzuia kufanya uamuzi (iwapo ungependa kupashwa tohara)” alisema.
chanzo: zanzibar24.
Comments