
Wengine 163 wamelazwa hospitali, 20 wakiwa na majeraha yanayohusiana na mvua kubwa.
Wanne wana majeraha mabaya.
Watu wapatao 300 wanadaiwa kukwamba katika hori ya Romero, mashariki mwa mji wa Santa Barbara.
Polisi wamesema eneo lililokumbwa na maporomoko hayo linafanana na "uwanja wa vita wakati wa Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia".
Mafuriko na maporomoko ya ardhi yameathiri baadhi ya maeneo ambayo
yaliathiriwa na moto mkubwa wa nyika na yameharibu barabara kuu ya pwani
umbali wa maili 30 (48km).
Maafisa wa uokoaji wamesema kuna watu kadha ambao hawajulikani waliko na kwamba idadi ya waliofariki inatarajiwa kupanda.

Maafisa
wa Kikosi cha Ulinzi Baharini wametuma ndege kadha kusaidia juhudi za
uokoaji na wametahadharisha umma dhidi ya kutumia ndege zisizo na
marubani kwani zitatatiza juhudi za uokoaji.
Maelfu ya wakazi wa California waliamrishwa kuondoka makwao
Jumatatu, mara ya pili katika kipindi cha miezi miwili. Mara ya kwanza
ilikuwa ni kwa sababu ya moto, wakati huu ni kwa sababu ya mvua.



chanzo:Bbc.
Comments