Kwa Yanga itakayocheza na Saint Louis FC ya Shelisheli, mchezo wa kwanza utapigwa Februari 10 Uwanja wa Taifa na utachezeshwa na waamuzi kutoka Ethiopia na Kamishna atatoka Namibia.
Taarifa ya CAF iliyosambazwa jana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ilisema mwamuzi wa kati atakuwa Belay Asserese, mwamuzi msaidizi namba moja Tigle Belachew namba mbili ni Kinfe Yilma. Mwamuzi wa akiba ni Amanuel Worku na Kamishna atakuwa Frans Mbidi.
Mchezo wa pili utakaochezwa Shelisheli kati ya Februari 20 na 21, utachezeshwa na waamuzi kutoka Madagascar na kamishna atatoka Mauritius.
Mwamuzi wa kati Andofetra Rakotojaona akisaidiwa na msaidizi namba moja Lionel Andrianantenaina na namba mbili Pierre Andrivoavonjy. Mwamuzi wa akiba Hamada Nampiandraza, Kamishna ni Ahmad Nazeer Bowud.
Pia waamuzi kutoka Sudan Kusini watachezesha mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya Simba na Gendarmerie Tnale ya Djibouti Februari 11 Uwanja wa Taifa.
Mwamuzi wa kati ni Alier James na msaidizi namba moja ni Abdallah Gassim na namba mbili ni Gasim Dehiya. Wa akiba ni Kalisto Gumesi. Kamishna anatoka Botswana ni Mmonwagotlhe Senai. Mchezo wa marudiano utakaochezwa Djibouti kati ya Februari 20 na 21 utachezeshwa na waamuzi kutoka Burundi na Kamishna atatoka Rwanda.
Mwamuzi wa kati ni Eric Manirakiza akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Pascal Ndimunzigo, namba mbili Willy Habimana. Mwamuzi wa akiba Pacifique Ndabihawenimana na kamishna Gaspard Kayijuka.
Comments