
Akizungumza Zanzibar24 Mwenyekiti wa baraza
hilo Khamis Rashid Kheir amesema vijana wamehamasika katika kufanya
shughuli za ujasiriamali ambazo zitawasaidia katika kujikwamua na
ukosefu wa ajira unaowakabili hivyo wameitaka serikali kuwasaidia
upatikanaji wa malighafi ili kuendelea na kazi zao.
Kwaupande wake Mjumbe wa baraza hilo Niki
Abdi Singano kutoka Shehia ya uzi amesema hali ya udhalishaji ipo
vizuri ikiwemo sabuni,shampuu,losheni na vitu vyengine lakini tatizo la
upatikanaji wa malighafi linawarudisha nyuma.
chanzo:Zanzibar24.
Comments