Balozi Seif akabidhi vifaa vya michezo timu 14 za soka Chumbuni.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amekabidhi vifaa vya michezo kwa Timu 14 za mchezo wa Soka  za Jimbo la Chumbuni vilivyotolewa na Uongozi wa Jimbo hilo vikilenga kuimarisha Sekta ya michezo kwa vijana wa eneo hilo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Balozi Seif akikabidhi vifaa vya Michezo kwa Mwakilishi wa Timu ya Soka ya G.S ya Shehia ya Karakana.
Vifaa hivyo ni miongoni mwa ahadi za Viongozi hao waliyoitoa wakati wa kampeni za uchaguzi kuelekea katika mnasaba wa kutekeleza vyema ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2015/2020.
Balozi Seif akimkabidhi Seti ya Jezi na Mipira Miwili Mwakilishi wa Timu ya Soka ya Chumbuzi City kwenye Mkutano wa Majumuisho hapo chuop cha Utalii Maruhubi.
Balozi Seif alikabidhi vifaa hivyo wakati akimaliza ziara yake ya kutwa moja katika Jimbo la Chumbuni kwenye Mkutano wa Majumuisho uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Balozi Seif akimkabidhi seti ya Jezi na Mipira Miwili Mwakilishi wa Timu ya Soka ya F.C Muembe Makumbi United.
Vifaa hivyo vinavyokadiriwa kugharimu zaidi ya shilingi Milioni Tatu ni pamoja na Seti ya Jezi na Mipira Miwili kwa Timu Tano kwa niaba ya nyengine 14 zilizomo ndani ya Jimbo hilo.
Mwakilishi wa Timu ya Soka ya F.C Jupiter iliyomo ndani ya Jimbo la Chumbuni akipokea Seti ya Jzi na Mipira Miwili kutoka kwa Balozi Seif vilivyotolewa na Uongozi wa Jimbo la Chumbuni.
 Akizungumza na wanajimbo hao Balozi Seif  ameupongeza mshikamano mkubwa unaoendelea kutawala ndani ya Jimbo la Chumbuni ambao unapunguza changamoto zinazowakabili watu wake.
Akitoa Taarifa katika Mkutano huo wa Majumuisho  Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza Maarufu Amjadi alisema Timu zote 14 za Soka kwenye Jimbo hilo tayari zimeshapata usajili wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar {ZFA}.
Amjadi alisema Uongozi wa Jimbo hilo utaendelea kuzihudumia Timu hizo katika masuala ya usajili, Vifaa pamoja na uwezeshaji ili ziweze kufanya vyema zinapoingia kwenye mashindano.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
24/1/2018.
chanzo:Zanzibar24

Comments