Uongozi
wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, umesema mshambuliaji wake, Obrey
Chirwa atareja nchini siku yoyote baada ya kwisha kwa msiba wa mtoto wa
Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina.
Chirwa
aliondoka nchini baada ya kuomba ruhusa kurejea kwao Zambia kwa masuala
ya kifamilia. Lakini baadaye akagoma kurejea nchini akitaka kumaliziwa
fedha zake za usajili.
Hali
hiyo ilisababisha hali ya sintofahamu na Chirwa akaendelea kubaki
Zambia huku akionekana mitandaoni akiendelea na kilimo cha mahindi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Salum Nyika amesema kilichomkwamisha Chirwa ni msiba wa mtoto wa kocha.
"Alikuwa
bado Zambia, baada ya kusikia kocha ana msimba, alilazimika kubaki kule
kumliwaza," alisema akionekana kutaka kupoza kidogo joto la Chirwa
kubaki Zambia kwa mgomo.
Hata
hivyo kumekuwa na taarifa kwamba, uongozi wa Yanga umemalizana naye kwa
kumpatia kiasi cha fedha zake za usajili na umekubaliana naye kurejea
haraka.
Comments