Majaliwa ametoa agizo hilo alipokuwa akizungumza
na wakazi wa vijiji vya Namahema ‘A’ na Namahema ‘B’ wilayani Ruangwa,
mkoani Lindi, baada ya kukagua mradi wa maji ambao unatarajiwa
kukamilika Januari 15, mwakani.
Hadi kukamilika kwake mradi huo utagharimu Sh. milioni 244.52, na
utahudumia wakazi 2,257 wa vijiji hivyo viwili ambao walikuwa
wanasongamana kupata maji kutoka kwenye kisima ambacho kilikuwa
kinatumia pampu ya mkono.
Waziri Mkuu yuko kwenye mapumziko ya mwisho wa mwaka, lakini ameanza ziara fupi ya siku tatu, kukagua miradi ya maendeleo jimboni kwake katika wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.
Jumla ya sh. milioni 189.93 zimeshatumika kwenye mradi huo ambazo ni sawa na asilimia 77.68 ya fedha ziliopangwa kutumika. Kijiji cha Namahema ‘A’ kina watu 1,668 na Namahema ‘B’ kina watu 589.
chanzo: zanzibar24.

Comments