
Akitoa hukumu hiyo leo Ijumaa katika kesi ya uhujumu uchumi namba
128/2016 hakimu wa mahakama hiyo, Ismael Ngaile amesema kila mshitakiwa
atahukumiwa kifungo cha miaka 25 jela na gari lao kutaifishwa liuzwe.
Mapema mwendesha mashitaka wa Jamhuri, Emmanuel Zumba ameiambia
Mahakama kuwa, washitakiwa hao walikamatwa Desemba 7, 2016 wakiwa kwenye
nyumba ya kulala wageni Serengeti wakiwa na mayai 16 ya mbuni yenye
thamani ya zaidi ya Sh 42 milioni ambayo waliyaficha ndani ya gari lao
kinyume cha sheria.
Amesema washitakiwa wakidai kuwa walikuwa wanapeleka nchini Kenya kwa ajili ya kuuza kwa watu wanaotengeneza dawa ya ukimwi.
chanzo: zanzibar24.
Comments