Wananchi watakiwa kulinda nguzo za umeme.

WA N A N C H I wanaoishi karibu na nguzo za umeme hapa nchini, wametakiwa kulinda kwa nguvu zao zote kwa kushirikiana na serikali za vijiji ambazo nguzo hizo zimepita kwani kwa kufanya hivyo kutasaidai kupunguza hujuma zinazoweza kujitokeza.
Meneja wa njia kuu za umeme nchini, Amos Kaihura alisema hayo wakati akizungumza na wananchi wa vijiji vya Mgongoro na Makomero, wilayani Igunga baada ya kutokea tatizo la kufunguliwa kwa njia ya umeme ya msongo mkubwa wa kilovati 400.
Alisema wananchi ndiyo wana jukumu ya kulinda miundombinu hiyo kwa sababu wao ndiyo wapo kwenye maeneo ambayo nguzo hizo zinapita na kuongeza kuwa hujuma hizo zimekuwa zikifanyika maeneo yao lakini wamekuwa hawatoi taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kuwadhibiti watu wanaofanya uhalifu huo.
Kaihura alisema kutokana na kufungua nguzo hizo, tatizo kubwa lingeweza kujitokeza nchini kwa wananchi wa mikoa ya Iringa, Dodoma, Singida, Tabora na mikoa ya Kanda ya Ziwa ingeweza kukosa umeme na kulisababishia taifa hasara kubwa.
Meneja huyo alisema serikali imewekeza kwa ajili ya wananchi kupata umeme wa uhakika lakini wahuni wachache wanataka kuharibu miundombinu ya umeme huo uliopo katika gridi ya taifa kutoka mkoani Iringa kwenda Kanda ya Ziwa
chanzo:Habarileo.

Comments