Wananchi wa mkoa wa mjini magharibi hawakuridhishwa na baa 14 zilizofungiwa na mahakama ya vileo.

Mahakama ya Vileo Zanzibar imezifungia baa 14 za Mkoa wa Mjini Magharibi  kutokana na kukosa  sifa  kisheria  ya kuendelea na biashara  ya Pombe kwa mwaka 2018.

Akitoa maamuzi hayo Mwenyekiti wa Mahakama hiyo Mohammed Subeit katika Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe  kufuatia makosa hayo sambamba na kukosa sifa hatua  ambayo  itapelekea baa hizo kutoendelea kufanyabiashara ya pombe kwa mwaka 2018 hadi 2019.


Akizitaja baa hizo  zilizokosa  vibali vya kuendelea na biashara  kwa Wilaya ya Mjini  na Magharibi B ni  Ras pub, Stone pub, na Valentine baa, Calfonia baa amani, Jambo Migombani, Jose pub , In baa, Golden stoo, Habital baa ya mitawi,titani na zebra kisauni amesema baa  hizo zimekosa sifa kutokana na mazingira yake na wamiliki wake hawafuati sheria za Vileo.

Aidha Subeit amewataka wamiliki wa baa waliokosa vibali kama hawakuridhishwa na uwamuzi wa mahakama ya wilaya  waende mahakama kuu kwa ajili ya kukata rufaa.

Kwaupande wake Katibu wa Kamati ya kupinga baa Zanzibar Abdalla Mnubi amesema amesikitishwa na maamuzi ya mahakama na Wananchi hawakurizika kutokana baa walizozipinga  hazikufungiwa  na hadi leo zinaleta  usumbufu mkubwa katika  makadhii ya Wananchi.

Mnubi amesema  licha ya Wananchi wa Mkoa wa Mjini  Magharibi kujitokeza kwa wingi  katika kutoa pingamizi zao mbele ya mahakama ya vileo lakini mahakama hiyo  haikujali na kuyatupilia mbali malalamiko yao juu ya baa hizo.

Aidha wametoa wito kwa serikali  kulisimamia suala la ongezeko la baa nchini  ambazo  huwaletea usumbufu Wananchi hasa zilizopo karibu na maakazi  pamoja na nyumba za ibada  zifungiwe ili kulinda maadili.

chanzo:Zanzibar24

Comments