Wanafunzi nchini wameshauriwa kuwacha kujiingiza katika makundi maovu ikiwemo kufanya mapenzi katika umri mdogo,mapenzi ya jinsia moja ambayo yatawaletea athari na kukatisha ndoto zao katika kutafuta elimu.
Akizungumza na Zanzibar24 baada ya utoaji wa elimu kwa wanafunzi wa skuli ya Mikindani dole Mkuu wa dawati la kijinsi la Polisi madema Kassim Fadhil Abdalla amesema nivyema wanafunzi kuwachana na matendo yasiyo na msingi badala yake kujikita katika masoma ili kujitengezea matokeo mazuri, yatayowaletea matunda baadae.
Kassim amesema katika skuli hiyo zimeanza kuonekana ishara mbaya kwa wanafunzi na tayari kesi zimeanza kuripotiwa katika madawati ya kijinsi kuhusu matendo maovu yanayofanyika katika skuli hiyo.
Kwaupande wao baadhi ya wanafunzi waliopata elimu hiyo Ruwaida Ahmada,Lailat Hamdani wametoa ushauri kwa wanafunzi wezao kuwatayari kubadilika na kutambua lengo walilolifata skuli na kuwacha kujiingiza katika vitendo viovu ambavyo vitawazalilishaji.
Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali duniani linatarajia kuadhimisha Siku 16 za kupiga udhalilishaji kwa wanawake na watoto ifikapo tarehe 8 mwezi huu.
chanzo:Zanzibar24
Comments