
Naibu Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Amali Zanzibar Mmanga Mjengo Mjawiri amewataka wajumbe wa
bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu Zanzibar kusimamia vyema marejesho ya
madeni ya fedha walizokopeshwa wanafunzi wa elimu ya juu ili kuipa uhai
bodi wa kuendelea kuwa na uwezo wa kutoa fedha hizo kila mda
utakapowadia.
Akizungumza wakati wa
uzinduaji wa bodi mpya ya awamu ya tatu ya mikopo ya elimu ya juu
huko mazizini amesema ili bodi hiyo iweze kujiendeleza lazima suala la
mrejesho wa fedha kusimamiwa na kupewa kipaumbe kwa bidii kubwa hasa
ukizingatia wahitaji wa mikopo bado wapo wengi na wanahitaji kupatiwa
fursa hiyo.
Amesema Zaidi ya Billion
35 zimetolewa na Serikali kwa njia ya mikopo na hadi sasa fedha hizo
zipo mikononi mwa wanafunzi wanaoendelea na masomo na wale
waliohitimu elimu ya juu hazijarejeshwa ambapo lisiposimamiwa na
kufanyiwa kazi litaweza kuzorotesha maendeleo na kuwakosesha wengine
fursa hiyo kupewa kwa ajli ya kujiendeleza.
Aidha Mjengo ameitaka
bodi hiyo kufanyakazi kwa mujibu wa sheria kwa kuzingatia miongozo
iliyopo ili kuleta ufanisi ambapo ameahidi kuwa serikali haitakuwa nyuma
katika ufuatiliaji wa mienendo ya utendaji kazi ya bodi hiyo.
Kwaupande wake
Mwenyekiti Mstaafuu wa awamu ya Pili Kombo Hassan Juma amewataka
watendaji hao kushirikiana na Wizara ya elimu katika kutafuta na kubuni
mbinu mpya zitakazowezesha kupatikana kwa fedha zitakazoweza kukidhi
mahitaji ya wanafunzi wa elimu ya juu na kuweza kujitegemea wenyewe.
Amesema Bodi bado
inakabiliwa na matatizo mengi ikiwemo Kasi ndogo ya makusanyo hivyo
nivyema kufanya jitihada za haraka kupambana ili kupata mafanikio
pamoja moja na kuandaa sera mahususi kwa wanafunzi wanaopata fursa za
kwenda kusoma nje ya nchi.
Aidha ameitaka bodi
kuharakisha marekejisho ya sheria ya bodi ya mikopo ili kuleta ufanisi
katika kazi za utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwani
iliyopo inamapungufu.
chanzo:Zanzibar24
Comments