
Rais Magufuli ameyasema hayo leo Desemba 18, 2017, kwenye Mkutano
Mkuu wa 9 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao unafanyika mjini Dodoma na
kusema kutokana na uimara wa CCM amepokea majina nane ya Madiwani wa
vyama vya upinzani na Mbunge mmoja ambapo wanasubiri muda tu kutangazwa.
“Nimepokea majina mengine ya viongozi wa upinzani ambao
wanataka kurudi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wasaidizi wangu wameniambia
yupo Mbunge mmoja anataka kurudi na ameniambia kuwa anataka kuja na
madiwani saba kwenye jimbo lake, nasema hiki ni kimbunga na wataisoma
namba kweli kweli.“amesema Rais Magufuli.
Hata hivyo, Rais Magufuli amesema kuwa CCM wataendelea kupokea na
kuwatangaza watu ambao wanahamia kwenye chama hicho na kudai kuwa lazima
kwanza wajiridhishe ili wasije kupokea na watu wengine ambao hawana
mpango mzuri kwa CCM.
Chanzo: zanzibar24.
Comments