Utoaji wa leseni za uwindaji wa kitalii sasa ni kwa mnada.

Wizara ya Maliasili na Utalii imeandaa Mkutano na wadau wa Sekta ya Uwindaji wa Kitalii ili kujadili mikakati ya kuimarisha sekta hiyo.
Hii ni pamoja na utekelezaji wa azma ya serikali ya kuanzisha utaratibu mpya wa utoaji wa leseni za vitalu vya uwindaji wa kitalii kwa njia ya mnada. 
Mwenyekiti wa Mkutano huo atakuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Hamisi A. Kigwangala, Wadau wote mnakaribishwa ili kufanikisha lengo la Mkutano huo kwa faida ya sekta ya uwindaji wa kitalii nchini na maliasili za nchi kwa ujumla.
Mkutano utafanyika tarehe 28 Desemba, 2017 saa nne asubuhi katika ukumbi wa LAPF, Dodoma.
chanzo:habarileo.

Comments