Mamlaka ya Udhibiti wa Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar imesema itasimamia kuhakikisha Mkandarasi aliyekuwa anafanya kazi ya utafiti wa gesi asilia baharini anawalipa fidia wavuvi walioharibiwa nyavu zao wakati wa zoezi hilo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mamlaka hiyo Omar Zuber amesema Mamlaka imekamilisha zoezi la utafutaji wa mafuta na gesi asilia baharini katika visiwa vya unguja na pemba lakini athari zilizojitokeza zitafanyiwa ufumbuzi kwa kulipwa fidia wavuvi hao.
Hata hivyo Omar amesema Zoezi hilo la utafiti wa mafuta na gesi asilia pia linatarajiwa kufanyika katika nchi kavu kwa baadhi ya maeneo na tayari baadhi ya vijiji vimesha orodheshwa kufanyika utafiti huo ikiwemo Jozani.
Amesema zoezi hilo litaweza kuwagusa watu wengi hasa wakulima wenye mashamba lakini Mamlaka imejipanga kikamilifu kuhakikisha utafiti wake hautoathiri kwa kiwango kikubwa lakini kama itatokea matatizo yoyote iweze kukabiliana nayo kwa ulipaji wa fidia ili kuwaondolea wananchi walalamiko.
Idadi ya mistari iliyofanyiwa utafiti ndani ya kitalu cha pemba Zanzibar ni 62,ambapo ilikuwa na kilomita 2482 na kwa nje ya kitalu ilikuwa mistari 4 na yenye kilomita 333.6.
CHANZO:Zanzibar24
Comments