Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Masoud Djuma
ameweka msimamo wake kuwa kikosi chake kitacheza kwa ushirikiano na
hakutakuwa na staa mkubwa kuliko timu.
Djuma ambaye anashikilia nafasi ya kocha
mkuu baada ya kufutwa kazi kwa Joseph Omog, amesema anapambana
kuhakikisha kikosi chake kinafanya vizuri kwa kushirikiana na wachezaji
wake lakini hatataka kuona kuna makundi.
“Kuwa na wachezaji ambao ni muhimu zaidi
ya wenzao, hili si jambo jema. Hakutakuwa na mambo hayo na zaidi
ningependa ushirikiano na upendo.
“Hii timu ni yetu sote, lazima kuwe na ushirikiano kuhakikisha tunafikia lengo na ndilo lengo la kila mmoja wetu,” alisema.
Kocha huyo raia wa Burundi, ametokea
Rayon Sports ya Rwanda ambayo alifanikiwa kuopa makombe mawili ya
ubingwa wa ligi na Kombe la Amani kama Kombe la Shirikisho hapa
nyumbani.
Comments