Rais
Uhuru Kenyatta wa Kenya amemuandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, kupinga kitendo cha mauaji ya
askari wake 15 waliokuwa wakilinda amani nchini Kongo, na kumpa pole
kufuatia msiba huo mkubwa.
Katika
barua hiyo, Rais Kenyatta amesema kushambuliwa kwa askari, ambao
walikuwa wakihudumia kwa sababu nzuri ya kuanzisha amani ya kudumu
nchini DRC ilikuwa mbaya, huku akiwapa pole watanzania na ndugu wa
marehemu, na kuwaombea wale waliojeruhiwa waweze kupona haraka.
Uhuru
Kenyatta ameendelea kwa kusema kwamba Kenya itaendelea kushirikiana na
watu na serikali ya Tanzania katika kulinda amani ya Kongo na maeneo ya
maziwa makuu, na kuangalia kesho bora ya maeneo hayo.
Rais
Kenyatta amesema Kenya inathamini jukumu muhimu lililofanywa na watunza
amani tangu imehusika katika mipango mingi ya kulinda amani.
Mwishoni
mwa wiki iliyopita askari 15 wa Tanzania waliokuwa wakilinda amani
nchini Kongo waliuawa na askari waasi wanaoendesha ampigano nchini humo,
huku 44 wakijeruhiwa, 8 wakiwa mahututi na wawili hawajulikani walipo.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments