
Akielezea uzinduzi wa kamati hiyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba jana wakati akizungumza na waandishi wa habari Mjini Dodoma, alisema Kamati ya mazingira itaundwa na wajumbe wenye uzoefu katika maeneo mbalimbali ya usimamizi wa mazingira.
“Kifungu namba 11 cha sheria ya mazingira kinasema itaanzishwa kamati ya Taifa ya ushauri wa mazingira itakayo mshauri Waziri kifungu namna 11;1 cha sheria kinasema itanzishwa Kamati ya taifa ya ushauri wa Mzingira itakayo mshauri waziri katika haya mamlaka ambayo nimeyazungumza,” alisema Makamba.
“Kamati ya mazingira itaundwa na wajumbe wenye uzoefu katika maeneo mbalimbali ya usimamizi wa mazingira kwenye sekta ya umma binafsi na vyama vya kiraia na kwamba iwe ni ya kitaalam.”
Katibu mkuu wa wizara hiyo, Joseph Malongo alisema kamati hiyo imeanzishwa kwa mujibu wa sheria na kwamba wananchi wanapaswa kujua na kuzingatia umuhimu wa mazingira katika kila jambo.
chanzo:zanzibar24.
Comments