
Katika Ujumbe wa twitter, bwana Trump alisema kuwa China ilionekana ''hadharani'' ikiruhusu mafuta hayo kwenda Korea Kaskazini.
Amesema
hakuwezi kuwa na suluhu ya kirafiki katika mgogoro wa Korea Kaskazini
iwapo mafuta yataruhusiwa kusafirishwa hadi Pyongyang.
China
mapema ilikana kwamba kumekuwa na ukiukaji wowote wa azimio la Umoja wa
mataifa la mafuta kati ya China na Korea Kaskazini.
Wiki iliopita ,
Beijing iliunga mkono azimio la Umoja wa Mataifa lililoandikwa na
Marekani ambalo lilishirikisha hatua za kupunguza kiwango cha mafuta
kinacheolekea Korea Kaskazini kwa asilimia 90.
Vikwazo hivyo vikali ni jaribio jipya kuzuia majaribio ya silaha yanyotekelezwa na Pyongyang.
Matamshi
hayo ya rais Trump dhidi ya China yanajiri baada ya gazeti moja la
Korea Kusini Chosun IIbo kuripoti kwamba meli za China zimekuwa
zikisafirisha mafuta kwa siri kupitia baharini kuelekea Korea Kaskazini.
Likiwanukuu
maafisa wa serikali ya Korea Kusini, limesema kuwa usafirishaji huo
unaenda kinyume na sheria kutoka meli moja hadi nyingine ulipigwa picha
na Satellite za Marekani za ujasusi takriban mara 30 tangu mwezi Oktoba.
Maafisa wa Marekani hawakuthibitisha ripoti hiyo lakini afisa ya
idara moja ya serikali aliyenukuliwa na reuters alisema kuwa
usafirishaji huo huenda unaendelea.
Usafrishaji wa mafuta kutoka
meli moja hadi nyingine unaendelea kuleta wasiwasi ikiwa miongoni mwa
njia za Korea Kaskazini kukwepa vikwazo hivyo.
China ambayo ni
mshirika mkubwa wa kibiashara wa taifa la Korea Kaskazini , imesema kuwa
inatekeleza vikwazo vyote vilivyowekwa na UN dhidi ya Korea Kaskazini.
Alipoulizwa maswali kuhusu ripoti za usafirishaji wa mafuta kutoka
meli moja hadi nyingine, msemaji wa wizara ya ulinzi nchini China Ren
Guoqiang aliambia maripota kwamba: hali ulioitaja haipo.
Msemaji
wa wizara ya maswala ya kigeni nchini Marekani Michael Cavey alisisitiza
kuhusu wito wa mataifa yote kusitisha uhusiano wa kiuchumi na Korea
Kaskazini.
''Tunatoa wito kwa China kusitisha uhusiano wowote wa
kiuchumi na Jamhuri ya kidemokrasi ya Korea Kaskazini ikiwemo utalii
pamoja na uuzaji wa mafuta ama bidhaa za mafuta'', alisema.

chanzo:Bbc.
Comments