Rais
Dkt. John Pombe Magufuli ameahidi kulipa madeni ya walimu takribani
shilingi Bil. 25 mara baada ya viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania
(CWT) kuthibitisha uhalali wa madeni hayo.
Rais
Dkt. Magufuli ametoa tamko hilo jana Mjini Dodoma ,alipokuwa akifungua
Mkutano Mkuu wa CWT ambao umehusisha wawakilishi kutoka Mikoa yote ya
Tanzania Bara .
“Ninawaahidi walimu wenzangu, mara baada ya zoezi la uhakiki kuisha wale walimu ambao wanadai malipo halali watalipwa,” alifafanua Rais Dkt. Magufuli.
Aliendelea
kusema kuwa kabla hajawa Rais alikuwa mwalimu hivyo anazifahamu vizuri
shida za walimu hivyo walimu wajisikie wana muwakilishi mzuri.
Aidha,
Rais Magufuli amewataka viongozi wa CWT wa wilaya na mikoa kuhakiki
madeni ya walimu ya maeneo yao na kuyawasilisha kwa Waziri Mkuu kwa
ajili ya kulipwa.
Rais
Dkt. Magufuli amesema Serikali ya awamu ya Tano imeendelea kufanya
jitihada za kuboresha maslahi ya walimu ambapo tangu imeingia madarakani
jumla ya shilingi bilioni 56.92 zimetolewa kwa ajili ya kulipa madeni
ya walimu ambapo kati ya fedha hizop, shilingi bilioni 14.23 ni madeni
ya mishahara na shilingi bilioni 42.69 ni madeni yasiyo ya mishahara.
Vile
vile Rais Magufuli amewasihi walimu wenzake kupokea kile kidogo ambacho
Serikali inakitoa wakati huu ambapo Serikali inawekeza katika
kutekeleza miradi mbalimbali kama vile miradi ya afya, umeme, maji,
barabara na reli. Miradi ambayo inawagusa pia walimu katika maisha yao
ya kila siku nawanapotimiza majukumu yao.
Wakati
huo huo, Rais Magufuli amewaahidi walimu hao kufanyia kazi maombi
mbalimbali ambayo wamewasilisha ikiwemo kurudisha posho ya kufundishia
pamoja na Serikali kutoa mikopo isiyo na riba ili kuwasaidia kujenga
nyumba za kuishi.
Hata
hivyo, amewata viongozi husika kushughulikia uwiano sahihi wa walimu wa
shule za msingi na sekondari walioko mijini na vijijini kutokana na
walimu wengi kupangiwa mijini.
Kwa
upande wake, Makamu wa Rais CWT Leah Ulaya alisema kuwa wanaimani na
Rais Magufuli na juhudi zake zinaonekana wazi katika kupambana na
ufisadi, uzembe, rushwa, uhujumu uchumi na vita dhidi ya madawa ya
kulevya.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments