Polepole alisema hayo jana wakati akihojiwa na
kituo kimoja cha Television na kusema hakuna mtu ambaye ametishwa kwa
kusema ukweli juu ya jambo fulani ambalo huenda lipo au linatokea
Tanzania.
“Hakuna mtu amezuiliwa kuongea ukweli ndani ya nchi ya
Tanzania, hakuna mtu ametishwa kwa kusema ukweli na hasa katika uongozi
wa awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, anayesema mtu
Tanzania kuna mtu kazuiliwa kuzungumza uhuru wake wa maoni nadhani
atakuwa na matatizo ila nachofahamu kwamba mtu kuzungumza lugha ya
matusi kwa mujibu wa Katiba yetu na sheria zetu ni makosa” alisema Polepole.
Polepole aliendelea kusisitiza kuwa viongozi hao wa dini wapo wazi na huru kusema chochote kile kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania “Wapo huru kusema chochote kwa mujibu wa Katiba yetu ya nchi na sheria za nchi na nitasema neno moja dogo kitu ambacho na mimi ninatoa rai, nitakapokaa vizuri nitafafanua vizuri mambo haya lakini ukiwa kiongozi yoyote yule kauli ni jambo la msingi sababu una watu wanakufuata” alisisitiza Polepole.
Jana Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani, Meja Jenerali Mst. Projest Rwegasira, ilitoa onyo na kuwataka viongozi wa jumuiya za kidini kutotumia mahubiri yao ya ibada kwa kufanya uchambuzi wa masuala ya siasa.
chanzo: zanzibar24.

Comments