Aliyekuwa
Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa wa Singida Kaskazini
aliyejiuzulu, Lazaro Nyalandu ameutaka Umoja wa Mataifa kuchukua hatua
zaidi juu ya kinachoendelea nchini Libya.
Amesema
kuwa ni lazima hatua zichukuliwe kwa kile kinachoendelea nchini Libya
ili kuweza kukomesha kile ambacho kinaendelea kwa sasa dhidi ya
binadamu.
“Umoja
wa Mataifa na Umoja wa Afrika lazima uchukue hatua dhidi ya Libya sasa.
tunachoshuhudia ni matusi kwa wanadamu,”amesema Nyalandu.
Aidha,
siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa zikiripotiwa kutoka Libya
kuwa kumekuwa na biashara ya utumwa ikifanyika ikihusisha Libya kuuza
Waafrika nchi za Ulaya.
Ubalozi
wa Libya nchini Tanzani umesema kuwa Waafrika wanaodaiwa kuuzwa kutoka
nchi hiyo, yawezekana walikuwa wanakabidhiwa kwa watoroshaji ili
wawapeleke Ulaya na sio kuwauza kama watumwa.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments