Mwili wa askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania Marehemu SGT Issa
Saleh Issa aliyekuwa majeruhi akipatiwa matibabu nchini Uganda baada ya
shambulio la Waasi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo utawasili katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Terminal I kesho saa
6:00 mchana.
Marehemu SGT Issa Saleh Issa alikuwa katika Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa nchini DRC.
Baada ya kuwasili kwa maiti hiyo, itapelekwa moja kwa moja Kijijini kwao Ndijani Wilaya ya Kati Mkoa Kusini Unguja kwa mazishi.
chanzo: zanzibar24.
Comments