Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amewateua wajumbe wa
bodi ya wakurugenzi wa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC).
Taarifa
kwa umma ya jana Alhamisi Desemba 7,2017 iliyotolewa na Naibu Katibu
Mkuu (Biashara na Uwekezaji), Profesa Joseph Buchweishaija imesema
uteuzi huo kwa kipindi cha miaka mitatu umeanza Desemba Mosi, 2017.
Uteuzi
huo umefanyika baada ya Desemba 6,2017 Rais John Magufuli, kumteua
Profesa Egid Mubofu kuwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa TFC
kuanzia Desemba Mosi, 2017.
Wajumbe
wa bodi walioteuliwa ni Nuru Angetile Ndile (Mchumi Mkuu, Wizara ya
Fedha na Mipango); Eli Nanyaro Pallangyo (Mkurugenzi Msaidizi, Wizara
ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji); Dk Kadida R.S. Mashaushi (Mhadhiri,
Chuo cha Usimamizi wa Fedha -IFM); na Peter Barnabas Shao (mshauri wa
masuala ya fedha katika kilimo).
Taarifa
imesema bodi hiyo itazinduliwa Desemba 11,2017 saa nne asubuhi katika
ofisi za Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji mjini Dodoma.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments