
Mlandege waliwachapa JKU mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa saa 8 za
mchana ambapo mabao ya Mlandege yamefungwa na Khamis Abuu dakika ya 18
na Abubakar Ame (Luiz) dakika ya 60 huku bao pekee la JKU limefungwa na
Khamis Abdallah katika dakika ya 34.
Nao Mwenge wamefanikiwa kuwachapa bao 1-0 timu ya Jamhuri kwenye
mchezo uliopigwa jioni ya leo huku bao pekee la Mwenge likifungwa na Ali
Salim Bajaka dakika ya 31 ya mchezo.
Badae saa 2:15 usiku utapigwa mchezo mwengine kati ya Taifa ya Jang’ombe dhidi ya Zimamoto kwenye uwanja wa Amaan.
Mashindano hayo yataendelea tena kesho kwa kupigwa michezo miwili katika uwanja wa Amaan.
Saa 10:00 za jioni Zimamoto watakuwa na kazi ngumu kucheza JKU na Saa 2:15 Taifa ya Jan’gombe watakipiga na Mlandege.
Chanzo:Zanzibar24.
Comments