
Akisomewa mashitaka hayo ya ubakaji katika kesi ya jinai namba
682/2017 mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya Tarime, Amon Kahimba,
Mwendesha Mashitaka wa Polisi Inspekta Saumu Ngoma alidai kuwa mtuhumiwa
Mariba alitenda makosa hayo kati ya ubakaji kwa nyakati tofauti kwa
wanafunzi wake wa darasa la kwanza na la pili kati ya Agosti na Novemba
mwaka huu 2017.
Mwendesha mashitaka alidai kuwa, wanafunzi hao wa kike chini ya
miaka 10 ambao majina yamehifadhiwa walibakwa na mwalimu huyo kwa
nyakati tofauti wakati wakiwa maeneo ya shule hiyo kwenye nyumba za
walimu.
Alidai mwalimu alikuwa akiwatuma na kisha wanapokuwa ndani ya nyumba alikuwa akitenda kosa hilo.
Chanzo- Habarileo na zanzibar24.
Chanzo- Habarileo na zanzibar24.
Comments