Mtumishi mgodi wa GGM akamatwa na Polisi kwa kutangaza mapenzi ya jinsia moja hadharani.

Wiki hii kumekuwa na video inasambaa mtandaoni ikiwaonesha wanawake wawili wakivishana pete huku wakipigana denda mbele ya umati wa wanaume.

Jeshi la Polisi Mkoani Geita limemshikilia mwanamke mmoja kati yao ambaye imebainika kuwa ni mtumishi wa mgodi wa GGM aliyetambulika kwa jina la Milembe Suleiman anayetuhumiwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema wanamshikilia kwa uchunguzi kwa kuwa kitendo walichokionesha ni kinyume cha utamaduni wa Kitanzania na Serikali ambayo imekuwa ikikemea na kupiga marufuku vitendo vya mapenzi ya jinsi moja.

Hata hivyo, Ofisa Habari wa GGM, Dili Tenga amesema hayo ni masuala binafsi ya mfanyakazi hivyo wao kama mgodi hawawezi kuyazungumzia lakini wanaviachia vyombo vya dola viendelee na uchunguzi wake.

Video hiyo pia haikuwachukiza watu wa kawaida tu kwani hata Mbunge wa Arusha mjini, Mhe Godbless Lema aliiposti kwenye ukurasa wake wa Twitter na kumtaka Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe Mwigulu Nchemba na IGP Simon Sirro kuchukua hatua haraka zaidi kuwakamata wahusika kwani kitendo hicho ni kinyume na sheria za nchi yetu.

chanzo: zanzibar24.

Comments