Mbunge
wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa amesema wanasiasa wanaohama
kutoka vyama vya upinzani kwenda CCM, wanafanya uamuzi huo kutokana na
uoga.
Msigwa
amesema hay oleo Ijumaa wakati akihojiwa katika kipindi cha Morning
Trumpet kilichorushwa na televisheni ya Azam akiwa na Mbunge wa Temeke,
(CUF) Abdallah Mtolea.
Msigwa
amesema kufanya siasa ndani ya CCM kuna urahisi kuliko kufanya nje ya
chama hicho kwa sababu unafanya siasa ukiwa unazungukwa na polisi na
unakuwa unalindwa lakini unapokuwa upinzani unakuwa kama yatima, hali
inayopelekea wengine waoga kushindwa na kuamua kwenda CCM.
“Hawa
wenzetu wanaochukuliwa mi naamini kuna uoga na kuna kununuliwa, mtu
akisema sisi wapinzani tuwananunua watu wa kutoka CCM, unawanunua watu
wa CCM waje kufanya nini upinzani, kuna mabomu, kuna dhiki, yani mtu
atoke CCM ambapo analindwa aje upinzani kwenye dhiki? Kwa hiyo hii
propaganda kuwa upinzani nao unanunua watu ni ya kutaka kupotosha umma
tu,” amesema Msigwa.
Msigwa
ameongeza kuwa gharama za kuwa upinzani ni kubwa ndio maana hata idadi
ya wanasiasa wanaohama kutoka upinzani kwenda CCM ni wengi kuliko
wanaotoka CCM kwenda upinzani na ndio maana hata baadhi ya wanasiasa hao
baada ya kuona hali ya joto kisiasa imezidi kuwa kali wametangaza
kurudi nyumbani CCM.
Akichangia
mada katika mjadala huo kuhusu wimbi la wanasiasa wanaohama vyama vya
siasa Mtolea alikosoa wanasiasa wanaohama vyama na kuacha ubunge kwa
kutoa sababu za kuunga mkono juhudi za Serikali.
“Hawa
wanaosema kwamba wamefurahishwa na kazi ya Rais, hivi kumuunga mkono
Rais ndio umtie hasara, kwa sababu ukijivua ubunge, jimbo lile unaliacha
wazi na uchaguzi lazima ufanywe kwa matakwa ya sheria, leo kurudia
uchaguzi kwa jimbo moja ni takriban Sh70bilioni, sasa Je unamsaidiaje
Rais kwa kuitia hasara Serikali kwa kurudia uchaguzi kwa gharama hizo.”
Mtolea
amesema baadhi ya wanasiasa waliotangaza kuondoka upinzani kwa kudai
upinzani umeishiwa ajenda, wasichokifahamu ni kwamba vyama vya siasa
haviendeshwi kwa ajenda bali vinaendeshwa kwa itikadi au misingi
iliyosababisha kuundwa kwa chama cha siasa ili waweze kumaliza kero
mbalimbali nchini na njia ya haraka ya kufikia maendeleo ya nchi.
Mtolea
alitolea mfano tatizo la kukatika kwa umeme kuwa linaweza kuwa ajenda
lakini tatizo hilo likiisha, ajenda hiyo inakua imekwisha, lakini
itikadi ya chama inabaki.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments