Mke
wa marehemu Bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita na mwenzake,
wanaokabiliwa na kesi ya mauaji ya dada wa bilionea huyo, Aneth Msuya,
bado wanaendelea kukaa mahabusu baada ya upande wa Jamhuri kudai
upelelezi haujakamilika.
Kesi hiyo ilitajwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.
Wakili
wa Serikali Mwandamizi, Patrick Mwita, alidai kuwa upelelezi wa kesi
hiyo bado haujakamilika na kuomba mahakama kupanga tarehe nyingine ya
kutajwa.
Hakimu
alisema kesi hiyo itatajwa Januari 8, 2018 na washtakiwa wataendelea
kukaa mahabusu.Mbali ya Miriam, mshtakiwa mwingine ni mfanyabiashara
Revocatus Muyela.
Katika
kesi ya msingi, washtakiwa wanadaiwa kuwa Mei 25, 2016 walimuua kwa
makusudi dada wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Aneth Msuya.
Chanzo:Mpekuziblog.
Comments