
Ahadi hiyo ameitoa
wakati akizungumza na viongozi wa UVCCM Taifa wakiongozwa na Mwenyekiti
Kheir James na Makamu Mwenyekiti Tabia Maulid Mwita, waliofika Afisi
Kuu ya CCM Zanzibar kwa ajili ya kutembelea na kuomba dua katika
kaburi la aliyekuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar
Marehemu Mzee Abeid Aman Karume .
Dk. Mabodi aliwambia
viongozi hao kwamba kumbukumbu na historia ya Marehemu Mzee Abeid
karume inatakiwa kulindwa na vijana wa CCM ambao wao ndio viongozi wa
sasa na baadae wenye dhamana ya kulinda serikali na Chama visichukuliwe
na wapinzani.
Naibu Katibu Mkuu huo amemtaja Marehemu Mzee Abeid Karume kuwa alikuwa ni kiongozi wa Mapinduzi mwenyekiti aliyekuwa naazna kubwa ya busara na falsafa pana ya masuala ya uongozi na ubunifu ndani na nje ya ASP na Serikali kwa ujumla.
Amesema Afisi Kuu ya
CCM Zanzibar inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti Dk.Ali Mohamed Shein
itatoa ushirikiano kwa UVCCM pamoja na jumuiya na taasisi zote za
kisiasa na kiserikali ili wananchi waendelee kupata huduma bora za
kijamii, kichumi na kisiasa.
Pia, ameueleza msafara
huo wa viongozi wa UVCCM waliofika Zanzibar kwa mara ya kwanza toka
wachaguliwe kupitia Mkutano Mkuu wa Tisa wa Umoja huo Taifa, kwamba
maendeleo yaliyopatikana visiwani Zanzibar yanatokana na juhudi za CCM
kuisimamia Serikali itekeleze Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015/2020.
“Kwanza karibuni sana
Kisiwandui ambapo ndio sehemu pekee yenye historia na Ofisi za waasisi
wetu wa Afro Shiraz Party (ASP), walioanzisha harakati za ukombozi wa
Waafrika wa visiwa vya Zanzibar na hatimaye Januari 12, 1964 wakaung’oa
utawala wa kisultani na kusimamisha Dola huru iliyojali maisha na utu
wa watu wote.
Nyinyi vijana ni azna
kubwa kwa chama chetu hivyo fanyeni kazi kwa ufanisi ili kulinda heshima
na dhamana mnazopewa kwa lengo la kuwanufaisha vijana wenzenu ambao
kwa njia moja ama nyingine hawajajaliwa kama zenu”, alisema Dk.Mabodi.
Naye Mwenyekiti wa
UVCCM Taifa , Kheir James amekipongeza Chama cha Mapinduzi Zanzibar
kwa juhudi zake za kuimarisha taasisi hiyo ya kisiasa licha ya kuwepo na
changamoto za kisiasa zinazosababishwa na wapinzani.
Mwenyekiti Kheir
amesema yupo tayari kufanya kazi na viongozi wa Chama cha Mapinduzi na
Serikali kwa ujumla ili changamoto mbali mbali zinazowakabili vijana
ziweze kupatiwa ufumbuzi wa kudumu na taasisi hizo.
chanzo: Zanzibar24.
Comments