MAYAGE kuagwa na kuzikwa leo alhamisi desemba 28, 2017; nyumbani kwake mbweni, eneo la maputo, dar es salaam.
Msiba uko nyumbani kwake Mbweni Kijijini, Dar es Salaam, eneo la Mbweni Maputo,siyo mbali na hospitali ya Mbweni Misheni.
Yaani
ukiwa unatokea Mwenge unapanda daladala ziendazo Mbweni Kijijini,
unashukia kituo cha Mbweni Misheni, kisha hatua chache mbele kuna njia
inayokwenda kushoto ituate barabara hiyo kwa kuongozwa na vibao
vinavyoelekeza msiba ulipo mpaka utakapofika nyumbani kwa marehemu,
ambaye ni maarufu kama Mzee Magazeti.
Njia nyingine ni kupanda mabasi ya Makumbusho-Bunju/Bagamoyo, shukia kituo cha Mianzini Bunju.
Hapo
chukua bodaboda kwa gharama ya kama 3000/= hadi mbele kidogo ya Mbweni
Misheni Hospitali. Ukifika hapo kata kushoto na muelekeze huyo bodaboda
afuate vibao vya kuelekeza msiba hadi nyumbani kwa marehemu.
Kwa wenye usafiri binfsi; unaweza kufika kwa njia mbili:
1.Ukitoka
Mwenge nenda mpaka Petrol Station ya Lake Oil eneo la Bunju. Hapo kuna
barabara ya lami kuelekea Mbweni. Ifuate hadi Mbweni
Kijijini,utakapoikuta Hospitali ya Misheni Mbweni. Baada ya hapo kata
kushoto.Fuata vibao vya msiba vitakufikisha.
2.Ukitoka
Mwenge nenda hadi njia panda Mbweni Jeshini, fuata njia ya daladala,
yapite mageti ya Jeshi hadi Mbweni Kijijini.Endelea mbele hadi Mbweni
Misheni Hospitali.Sogea mbele kidogo, halafu kata kushoto na anza
kufuata maelekezo ya vibao vya msiba ambavyo vitakufikisha.
Usafiri kwa Wanahabari
Kwa mujibu kamati ya maandalizi kutakuwa na mabasi mawili ya UDA yatakayobeba wanahabari watakaokwenda kumuaga mwenzao.
Basi
la kwanza litakuwa Idara ya Habari Maelezo,Mtaa wa Samora, kuanzia saa
1:30 asubuhi ambapo litaondoka saa 2:30 kuelekea msibani Mbweni.
Basi
la pili litakuwa Mwenge,maeneo ya kituo cha mafuta cha BP, kuanzia saa
mbili asubuhi ambapo litaondoka hapo saa 3 kuelekea msibani.
Poleni sana,
Imetolewa na Kamati ya Maandalizi
Desemba 27, 2017.
Comments