Aliyekuwa
mgombea urais 2015 kupitia ACT - Wazalendo Mama Anna Mghwira ambaye kwa
sasa ni mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, ametangaza rasmi kujiunga na chama
cha Mapinduzi CCM.
Tukio
hilo limetokea leo mjini Dodoma kwenye uzinduzi wa mkutano wa Umoja wa
Wanawake Tanzania wa CCM (UWT), ambao umehudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Katika
mkutano huo mama Anna Mghwira amesema ameamua kufanya hivyo baada ya
kuona jitihada za CCM katika kuleta maendeleo, hivyo akaona ni vyema
akajiunga nao.
"Mimi
baada ya kuwa Mkuu wa Mkoa kwa muda mfupi nimeona mengi ndani ya CCM na
nimeona sio mbaya nikitamka kuwa naungana nanyi rasmi, ahsanteni sana
kwa kunipokea na kama niliposikia hotuba ya Mwenyekiti ni kweli kuwa
sisi akina mama ndiyo wenye jukumu la kubeba nchi. Na mimi naungana na
akina mama wenzangu wa UWT wenye malengo ya kuendeleza taifa", amesema mama Anna Mghwira.
Mama Anna Mghwira anakuwa kiongozi mkubwa wa tatu kitaifa wa ACT Wazalendo kujiunga na CCM ndani ya mwaka huu.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments