
Sheikh Ponda ameachiwa huru mbele ya Jaji Johnson Mkasimongwa ambaye
amesema anakubaliana na uamuzi wa Mahakama ya Morogoro kumuachia huru
Sheikh Ponda katika kesi ya kutoa matamshi ya uchochezi.
“Mahakama ya Morogoro haikukosea kumuachia huru Sheikh Ponda na mimi nakubaliana na uamuzi huo, hivyo namuachia huru,” amesema Jaji Mkasimongwa
Miongoni mwa hoja alizozitoa Jaji Mkasimongwa ni kwamba upande wa
Jamhuri haikupaswa kumshtaki Sheikh Ponda kwa kosa lile la kuvunja amri
ya Mahakama ya Kisutu bali ilitakiwa wamrudishe katika Mahakama hiyo ili
imchukulie hatua zaidi.
Mashtaka yaliyokuwa yakimkabili Sheikh Ponda katika Mahakama ya
Morogoro, anadaiwa August 10, 2013, katika eneo la Uwanja wa Ndege,
Manispaa ya Morogoro, Ponda aliwaambia Waislamu wasikubali uundwaji wa
kamati za ulinzi na usalama za misikiti, kwa madai kuwa zimeundwa na
BAKWATA, ambao ni vibaraka wa CCM na serikali hivyo aliwaagiza waumini
hao endapo watu hao watajitokeza kwao na kujitabulisha kwamba ni kamati
za ulinzi na usalama za misikiti, wafunge milango na madirisha wawapige.
Ilielezwa kuwa kauli hiyo ni kinyume cha agizo la Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu, iliyotolewa na Hakimu Victoria Nongwa May 9, 2010, ambayo
ilimtaka Ponda ndani ya mwaka mzima kuhubiri amani na Kuwa Raia Mwema.
Kosa jingine inadaiwa August 10, 2013 katika eneo la Uwanja wa
Ndege, Morogoro, Ponda aliwaambia Waislamu kuwa serikali ilipeleka jeshi
Mtwara kushughulikia suala la vurugu iliyotokana na gesi ili kuwaua,
kuwabaka na kuwatesa wananchi, kwa sababu asilimia 90 ya wakazi hao ni
Waislamu.
chanzo: zanzibar24.
Comments