
Yisrael
Katz alisema kuwa anataka kumpa hushima rais huyo wa Marekani kufuatia
uamuzi wake wa kutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.
Ukuta wa Magharibi ndilo eneo takakatifu zaidi ambapo wayahudi wanaruhusiwa kuomba.
Reli
hiyo mpya ya chini kwa chini na kituo cha treni na sehemu ya mradi wa
reli ya mwendo kasi kutoka Tel Aviv ambayo inatarajiwa kuzinduliwa mwaka
ujao.
Ujenzi wa awali eneo lililo karibu na Ukuta wa Magharibi
ambalo hujulikana kwa waislamu kama Haram al-Sharif na kwa wayahudi kama
Temple Mount imezua maandamano kutoka kwa wapalestina.
Bw. Katz aliliambia gazeti moja la Israel la Yedioth Ahronoth kuwa
kuongezwa kwa reli kutoka Tel Aviv kwenda Jurusalem ndio mradi muhimu
zaidi kwa wizara ya uchukuzi.
Alisema kuwa ameidhinisha pendekezo
kwa kamati ya reli ya Israel ya kujenga reli ya chini kwa chini ya
umbali wa kilomita 3 kutoka Binyanei HaUma magharibi mwa Jerusalem
kwenda Ukuta wa Magharibi iliyo eneo linalokaliwa na Jerusalem
Mashariki.
Hali ya mji wa Jerusalem ndio chanzo cha mzozo kati ya Israel na Palestina.
Israel
inautaja mji wa Jerusalem kuwa mji wake mkuu huku wapalestina
wakilitaja eneo la Jerusalem Mashariki lililotwaliwa na Israel wakati wa
vita vya mwaka 1967 kama mji mkuu wa taifa lake la baadaye.
chanzo:bbc.
Comments