Kesi ya vigogo wa IPTL yaahirishwa hadi Desemba 22.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo ijumaa Desemba 8, 2017, imeahirisha kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mmiliki wa Kampuni ya kufua umeme ya IPTL, Harbinder Singh Sethi na Mfanyabiashara, James Rugemarila hadi Desemba 22, 2017, kutokana na upelelezi wa kesi hiyo kutokamilika.

Harbinder Singh Sethi pamoja na Mfanyabiashara James Rugemarila, kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12 yakiwemo ya kutakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya zaidi ya Bilioni 3.


chanzo: zanzibar24.

Comments