Karibu watu 200,000 wakimbia moto wa nyika California.
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
Karibu watu 200,000 kwa sasa
wamehamishwa kufuatia moto wa nyika huko California huku makundi ya
uokozi Wazima moto 5,000 wamekuwa wakipambana na moto huo ambao
umeharibu mamia ya nyumba kusini mwa jimbo la California.
Idadi ya watu waliohamishwa iliongezeka karibu mara nne siku ya Ijumaa baada ya moto wa tano kuzuka kaskazini mwa San Diego.
Wazima moto wakiondoa bidhaa kutoka kwenye nyumba za watu.
Kifo kimoja kimeripotiwa hadi sasa baada ya mwanamke mmoja kupatikana eneo lililokuwa limeteketea katika kaunti ya Ventura.
Hadi Alhamisi jioni, idara ya moto ya California ilisema kuwa moto ulilazimu kuhamishwa kwa watu 189,000.
Nyumba nyingi zilizo kwenye hatari ni za mamilioni ya dola
Gavana wa California Jerry Brown ametangaza hali ya tahadhari eneo hilo.
Ikulu ya White House nayo inasema itatoa msaada wowote unaohitajika.
Upepo wenye joto wa Santa Ana wa jangwani umesababisha moto huo kuongezeka zaidi.
Comments