Kampuni ya Acacia kuuza baadhi ya mali zake.

Kampuni ya Madini ya Acacia imesema kuwa itaiuzia Kampuni ya Dhahabu ya Sandstorm, asilimia 2 ya mrahaba wake katika mgodi wa Houndé uliopo nchini Bukinafaso kwa dola za kimarekani 45 milioni sawa na shilingi za kitanzania 100 bilioni.
Mpango huo unatarajiwa kufungwa mapema katika robo ya kwanza ya mwaka 2018.
Acacia, ambayo ina migodi mitatu ya dhahabu nchni Tanzania, imeathiriwa na mabadiliko ya sheria za madini ambazo zimevutia rufaa ya uwekezaji wa kampuni hizo zenye makao yake nchini Afrika Kusini na Tanzania, ambapo mataifa hayo yanahisi kuwa hawafaidiki kutokana na madini yao.
Kampuni ya Dhahabu ya Barrick ambayo ndiyo kubwa zaidi duniani kwa uchimbaji wa madini ya dhahabu na inamilikiwa na Acacia kwa asilimia 63.9, iliingia katika mvutano na serikali ya Tanzania , jambo ambalo lilipelekea Acacia kulipa dola za kimarekani 300 milioni kwa nchi ya Tanzania.
Acacia ilieleza kuwa haitoweza kumudu gharama hizo kwa wakati mmoja.
Uuzaji wa mrahaba huo utasaidia kuimarisha hali ya kifedha ya kampuni hiyo ambayo inaingia mwaka wa pili sasa tangu ilipozuiliwa kusafirisha nje ya nchi mchanga wa madini (makinikia).
chanzo:zanzibar24.

Comments