“Kwa wafungwa waliobaki gerezani wao nao waishi kwa amani, wafanye kazi warekebishike, kwahiyo kwa sasa hata wale wafungwa wa vifungo virefu ambao tulikuwa hatuwatumii huko nyuma kwa kuogopa mambo mbalimbali lakini sasa hivi watakuwa wamejifunza katika hili kwamba ukiishi gerezani ukirekebishika mheshimiwa Rais yupo atatumia mamlaka yake kama alivyopewa na atawasamehe kama alivyowasamehe wengine”, amesema Kamishna Malewa.
Kamishna Malewa pia amemuelezea Nguza Viking (Babu Seya ) na kusema kuwa alikuwa mfungwa mwenye nidhamu sana na alipewa cheo kikubwa gerezani yaani Unyampara mwaka mmoja tu alivyoingia gerezani.
Desemba 9, mwaka huu siku ya uhuru kwa mujibu wa ibara ya 45 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Rais John Pombe Magufuli alitoa msamaha kwa wafungwa 61 waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa na wawili Nguza Viking (Babu Seya ) na Johnson Nguza (Papii Kocha ) waliohukumiwa kifungo cha maisha jela.
chanzo:zanzibar24.
Comments