
Katika mahojiano na kipindi cha Maisha Mseto cha Times Fm, Jerry
amesema kutokana na uwezo wake suala la ubunge kwake ni jambo rahisi tu
sawa na kubofya button.
“Mimi Jerry Muro mmoja ni sawa na wabunge 10 wa Chadema,
nimewazidi kifikra, kinguvu, kipesa, maadili, kihoja na mambo mengine
mengi sana” amesema Jerry.
Katika hatua nyingine Jerry amesema mwaka 2020 si ajabu kwa
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na mjumbe wa kamati kuu ya chama
hicho, Edward Lowassa wakirejea katika Chama cha Mapinduzi (CCM).
chanzo: zanzibar24.
Comments