
Leo Alhamisi, Desemba 28, 2017 kupitia kipindi cha Joto la Asubuhi
cha Radio E-FM, Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais (Ikulu),
Gerson Msigwa, amesema kuwa hana taarifa yoyote juu ya tuzo hiyo.
“Mimi sina taarifa zozote kwa sababu mtu anapotoa tuzo si
lazima awasiliane na mtu anayempa tuzo, wao wanakuwa na vigezo vyao
kadiri ya watu walivyowapima viongozi. Mimi sina information zozote kwa
hiyo ni vizuri mngewatafuta hao Nelson Mandela wenyewe hicho chuo
waweze kuwaeleza tuzo hizo taarifa wanakuwa nazo vyuo wenyewe,“ amesisitiza Msigwa.
Hata hivyo tayari Wakfu wa Nelson Mandela nchini Afrika Kusini
umebainisha kuwa haukuandaa, kusimamia wala kutoa tuzo hizo, ambazo
zimeripotiwa katika vyombo mbalimbali ya habari nchini Tanzania, Kenya
na Burundi jana Desemba 27, 2017.
chanzo: zanzibar24.
Comments