
Pamoja na hayo, pia atapewa watumishi 20, wakiwemo walinzi wake 6
watakaokuwa wanalipwa na serikali ya nchi hiyo, kwa mujibu wa gazeti la
serikali la Herald.
Rais Mugabe mwenye umri wa miaka 93, aliyejiuzulu nafasi yake ya
urais nchini Zimbabwe, ndiye kiongozi wa kwanza kutajwa kunufaika na
mikakati hiyo mipya iliyotangazwa na Rais Emmerson Mnangagwa.
hakuna tarifa zilizotolewa kuhusu malipo, lakini katiba ya nchi hiyo
inataja kuwa Rais Mstaafu atalipwa pensheni ambayo ni sawa na mshahara
wa Rais aliyepo madarakani kwa wakati huo.
Mwezi uliopita, chombo kimoja cha habari nchini Zimbabwe kiliripoti
kuwa Mugabe aliahidiwa fedha kiasi cha dola za kimarekani 10 milioni
(sawa na shilingi za kitanzania 22.3 bilioni) kama nyongeza ya kustaafu
ikiwa ni moja ya vitu alivyoahidiwa ili ajiuzulu. Serikali ya Zimbabwe
ilipinga vikali madai haya.
Kama sehemu ya stahiki zake, Rais Mugabe atapewa gari aina ya
Mercedes Benz s500 pamoja na mengine mawili ambayo yatakuwa
yakibadilishwa kila baada ya miaka mitano.
Mugabe na mkewe Grace watapewa pasi za kusafiria za kidiplomasia
ambazo zitawaruhusu kusafiri safari nne za ndege au treni katika daraja
la kwanza (first class) na safari nne za nje ya nchi kwa kutumia ndege
binafsi.
Vilevile atapewa nyumba iliyokamilika katika eneo lolote atakalotaka
ndani ya Mji Mkuu Harare. Nyumba hiyo italipiwa gharama zote na
serikali.
Pia, atapata bima ya Afya yeye pamoja na mkewe na wengine wanaomtegemea.
chanzo: zanzibar24.
Comments